• HABARI MPYA

    Tuesday, November 19, 2013

    YANGA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI KOMBE LA UHAI…MWENDO ULE ULE, KIDUDE NA HAINA KUCHOMOA

    Na Prince Akbar, Ilala
    YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, maarufu kama Kombe la Uhai baada ya asubuhi hii kuilaza Coastal Union ya Tanga bao 1-0, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
    Shujaa wa Yanga SC leo alikuwa ni Hamisi Issa aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 67 akimalizia pasi ya Hassan Kidishi.
    Shujaa wa Yanga B leo, Hamisi Issa akiwapungia mashabiki baada ya kufunga

    Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Watoto hao wa Jangwani, baada ya awali kuilaza Mbeya City bao 1-0 kwenye Uwanja huo huo.
    Kocha wa Yanga B, Salvatory Edward Augustino ‘Doctor’ alifurahishwa na matokeo hayo na kusema kwamba vijana wake wamecheza mechi ngumu mno mwanzoni, lakini wamefanikiwa kushinda.
    “Kama ambavyo umeona mechi zetu zote tulizocheza ni ngumu, Mbeya City ni timu nzuri sana na leo Coastal umewaona ni wazuri, lakini wote tumewafunga, nina kila sababu ya kuwapongeza vijana wangu,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Yanga.
    Wakati Yanga iliifunga Mbeya City 1-0 katika mchezo wa kwanza, Coastal Union nayo iliilaza Azam FC mabao 2-1. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI KOMBE LA UHAI…MWENDO ULE ULE, KIDUDE NA HAINA KUCHOMOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top