• HABARI MPYA

  Friday, October 04, 2019

  MSUVA APIGA BONGE LA BAO KATIKA BIRTHDAY YAKE DIFAA EL-JADIDI YACHAPA 1-0 FAR RABAT

  Na Mwandishi Wetu, RABAT
  BAO pekee la kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana lilitosha kuipa Difaa Hassan El-Jadidi ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, FAR Rabat katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Morocco Uwanja wa Manispaa ya Kenitra.
  Simon Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC ya Dar es Salaam, alifunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 23 katika siku ambayo alikuwa anasherehekea kutmiza miaka 26 tangu azaliwe Oktoba 2, mwaka 1993. 
  Msuva ambaye katika timu hiyo yupo pamoja na chipukizi mwingine Mtanzania, Nickson Kibabage aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mtibwa Sugar jana alicheza vizuri mno.
  Simon Msuva akikimbia kushanglia na wachezaji wenzake baada ya kuifungia bao pekee Difaa Hassan El-Jadidi ikiilaza 1-0 FAR Rabat jana


  Na baada ya mchezo huo, wachezaji wa Difaa Hassan El-Jadidi walianza kumuimba nyota hiyo wa Tanzania hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo. 
  Difaa Hassan El-Jadidi watateremka tena dimbani, Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan Jumapili kumenyana na Wydad Casablanca katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco kuanzia Saa 3:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA APIGA BONGE LA BAO KATIKA BIRTHDAY YAKE DIFAA EL-JADIDI YACHAPA 1-0 FAR RABAT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top