• HABARI MPYA

    Friday, March 09, 2018

    SIMBA NA AL MASRY YAINGIZA MILIONI 85, SIMBA YAAMBULIA MILIONI 43 BAADA YA MAKATO KIBAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHEZO wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC ya Tanzania na Al Masry ya Misri uliochezwa Jumatano wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza jumla ya Sh. 85,045,000.
    Kiasi hicho cha fedha kimetokana na jumla ya watazamaji 14,798 waliojitokeza kuushuhudia mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
    Katika watazamaji hao 14,798 ni 250 tu walioketi jukwaa la VIP A ambako kiingilio chake kilikuwa Sh. 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000, watazamaji 557 waliketi VIP B na C ambako viingilio vyake vilikuwa Sh 15,000 na kapatikana jumla ya Sh 8,355,000.
    Sehemu ya mashabiki wa Simba waliojitokeza Uwanja wa Taifa juzi timu yao ikimenyana na Al Masry

    Kwenye majukwa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani ndiko waliingia watazamaji wengi zaidi, 13,644 kwa kiingilio cha Sh. 5,000 ambako zimepatikana jumla ya Sh. 68,220,000.
    Katika fedha hizo Sh. 12,972,966.10 imekatwa Kodi (VAT), 5,017,655.00 imeenda kwa Selcom waliokuwa wakikusanya mapato, TFF wamepata Sh. 3,352,718.94, Uwanja Sh. 10,058,156.83, Gharama za mchezo Sh. 6,034,894.10, BMT  670,543.79 na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepata Sh. 3,352,718.94 wakati klabu ya Simba, imepata Sh. 43,585,346.28.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA AL MASRY YAINGIZA MILIONI 85, SIMBA YAAMBULIA MILIONI 43 BAADA YA MAKATO KIBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top