• HABARI MPYA

  Wednesday, March 07, 2018

  MBEYA CITY YAIBAMIZA MBAO FC 2-0 SOKOINE, SINGIDA UNITED CHUPUCHUPU KUPAPASWA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Mbao FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. 
  Ushindi huo unaifanya Mbeya City ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, wakati Mbao FC inabaki nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya timu 16, kwa pointi zake 19 za mechi 21 pia. 
  Mabao ya Mbeya City mchezo wa leo yamefungwa na beki wake hodari, John Kabanda dakika ya 28 na mshambuliaji Eliud Ambokike dakika ya 47, ambaye hilo linakuwa bao lake la tisa msimu huu.
  Eliud Ambokike leo amefunga bao lake la tisa msimu huu wa Ligi Kuu Mbeya City ikiichapa Mbao FC 2-1

  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Singida United imelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Namfua mjini Singida. 
  Ruvu Shooting walitangulia kwa bao la Issa Kanduru dakika ya tisa, kabla ya beki Kennedy Wilson kuisawazishia Singida dakika ya 73.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAIBAMIZA MBAO FC 2-0 SOKOINE, SINGIDA UNITED CHUPUCHUPU KUPAPASWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top