• HABARI MPYA

  Friday, March 16, 2018

  LIPULI YAPANIA KUMALIZIA VIZURI LIGI KUU, YAWEKA MKAKATI WA KUSHINDA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Lipuli FC, umeweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara. 
  Lipuli ambao wameweka mikakati ya kushinda michezo miwili ya Mbao na Mwadui iliyopo mbele yao watakaocheza ugenini.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online, Mwenyekiti wa timu hiyo, Ramadhani Mahano alisema wanatambua nafasi waliyopo wasipokuwa makini kushinda mechi zilizosalia huenda wakawa na wakati mgumu.
  Alisema wametoa mapumziko ya siku chache kwa wachezaji wao, ila wameenda wakiwa na mikakati ya kupata ushindi katika michezo iliyopo mbele yao. 
  "Tunatambua ugumu wa ligi, hivyo  tunatakiwa kujipanga kuhakikisha tunashinda michezo yetu dhidi ya Mbao na Mwadui ambao tutacheza ugenini," alisema.
  Mahano alisema wasipokuwa makini katika michezo hiyo na watakuwa katika wakati mgumu.
  Kwa sasa Lipuli inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa na pointi 27 za mechi 22, ikizidiwa pointi 19 na vinara, Simba na Yanga wenye pointi 46 kila mmoja. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI YAPANIA KUMALIZIA VIZURI LIGI KUU, YAWEKA MKAKATI WA KUSHINDA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top