• HABARI MPYA

  Friday, March 16, 2018

  AALIYAH WA BEINTEHAA AJA KUUPAMBA USIKU WA SZIFF APRILI 1 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSANII wa kihindi wa kike, Preetika Rao maarufu kama 'Aaliyah' atakuwa miongoni mwa wageni maalum katika usiku wa tuzo za filamu Tanzania, ujulikanao kama SZIFF utakaofanyika Aprili 1, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam.
  Aaliyah alijizolea umaarufu na kupenda na wengi hapa nchini kupitia tamthiliya ya Beintehaa ambayo imekuwa ikirushwa na Televisheni ya Azam katika lugha ya Kiswahili baada ya kutafsiriwa.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Kampuni hiyo, Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando amesema kwamba licha ya Aaliyah pia kutakuwa na wasanii wengine maarufu watakaokuja kushuhudia tuzo hiyo.
  Preetika Rao anakuja kuupamba usiku wa SZIFF Aprili 1, mwaka huu Mlimani City mjini Dar es Salaam

  Amesema tuzo hizo kubwa za kwanza kufanyika hapa nchini ni maalum kuibua vipaji vya wasanii na kuendeleza tasnia ya sanaa ya maigizo na filamu kwa ujumla Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
  "Filamu hizo kutoka nchini zilizotajwa zinazowania vipengele hivyo na kuondoka na Tuzo, fedha taslimu na utambulisho maalum na wakipekee kwenye soko la filamu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara " alisema Muhando.
  Alisema katika tuzo hiyo kutakuwa na filamu bora, mwandishi bora wa filamu na  msainii bora wa kika na kiume.
  Aliyah atapata nafasi ya kwenda Visiwani zanzibar kwa ajili ya kuzungumza na wasanii wa huko pamoja na hapa nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo.
  Mkurugenzi Mratibu wa vipindi wa Uhai Production, Yahya Kimaro akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu Azam Media,Tido Mhando (wa pili kushoto) kabla ya kutangaza vipengele 18 vya tuzo za SZIFF 
  Mkurugenzi Mkuu Azam Media Limited,Tido Mhando (kushoto) akijadiliana jambo na Jaji Mkuu wa shindano la SZIF 
  Msimamizi wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AALIYAH WA BEINTEHAA AJA KUUPAMBA USIKU WA SZIFF APRILI 1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top