• HABARI MPYA

  Friday, February 09, 2018

  COUTINHO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO BARCA YASHINDA 2-0

  Kiungo Mbrazil, Philippe Coutinho akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 49 Uwanja wa Mestalla mjini Valencia kufuatia kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Andre Gomes katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme. Hilo ni bao la kwanza kwa Coutinho tangu asajiliwe mwezi uliopita kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 145 kutoka Liverpool wakati bao la pili lilifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 82 na wote walifunga kwa pasi za Luis Suarez. Barca inaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya Februari 1 kushinda 1-0 Camp Nou bao la Suarez pasi ya Lionel Messi dakika ya 67 na sasa itakutana na Sevilla iliyotoa Leganes kwa jumla ya mabao 3-1, sare ya 1-1 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COUTINHO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO BARCA YASHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top