Kiungo Mbrazil, Philippe Coutinho akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 49 Uwanja wa Mestalla mjini Valencia kufuatia kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Andre Gomes katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme. Hilo ni bao la kwanza kwa Coutinho tangu asajiliwe mwezi uliopita kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 145 kutoka Liverpool wakati bao la pili lilifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 82 na wote walifunga kwa pasi za Luis Suarez. Barca inaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya Februari 1 kushinda 1-0 Camp Nou bao la Suarez pasi ya Lionel Messi dakika ya 67 na sasa itakutana na Sevilla iliyotoa Leganes kwa jumla ya mabao 3-1, sare ya 1-1 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Tributes paid after Spanish top-flight football manager and three of his
children are feared dead in tourist boat rough seas drowning
-
Rescuers are searching for Fernando Martin, who trains Valencia's Women's B
team, and his three children Elia, 12, Kike, 10, and Mateo, nine.
1 hour ago



.png)
0 comments:
Post a Comment