• HABARI MPYA

  Saturday, January 13, 2018

  ZIDANE ANACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA REAL MADRID

  REAL MADRID inatafuta mbadala wa wa Zinedine Zidane, ingawa kocha huyo Mfaransa hana wasiwasi licha ya taarifa nchini Hispania kusema Joachim Low anatarajiwa kuchukua nafasi.
  Kitendo cha Real Madrid ya Zidane kushindwa kuifunga timu ya Daraja la pili, Numancia Jumanne usiku wiki hii wakitoa sare ya 2-2 katika mchezo wa marudiano wa kombe la Mfalme kunazidi kuchochea mabadiliko ya bencho la Ufundi Santiago Bernabeu.
  Kiwango cha kimezidi kushuka na baada ya kufungwa nyumbani na Barcelona na kutoa sare ugenini na Celta Vigo sasa wanazidiwa pointi 16 na vinara wa ligi kutoka Katalunya. Wanashika nafasi ya nne na ni pointi tu inayowaondoa kwenye la timu zilizo hatarini kushuka Daraja.
  Pamoja na kocha Zinedine Zidane kuipa mataji matano Real Madrid mwaka 2017, lakini sasa anaweza kuondolewa

  Kwenye Ligi ya Mabingwa walifungwa na Tottenham Uwanja wa Wembley na kwa kushindwa kuongoza kundi sasa watakutana na timu ngumu, Paris Saint-Germain kwenye hatua ya 16 Bpra  Februari 14 Uwanja wa Santiago Bernabeu.
  Lakini Zidane ana hazina ya kutosha benki baada ya kuipa timu mataji matano msimu mwaka 2017. Mjerumani Low amekuwa akitakiwa na Madrid kwa muda sasa, lakini wakati wote amekuwa akisema anapenda kuendelea kufundisha timu ya taifa. 
  Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2020, maana yake Madrid itatakiwa kumnunua.
  Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino na wa Chelsea, Antonio Conte pia wanatajwa kuhamia Man City pamoja na Thomas Tuchel na Unai Emery.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE ANACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top