• HABARI MPYA

  Sunday, January 07, 2018

  YANGA YAENDELEZA UBABE KOMBE LA MAPINDUZI, YAIZIMA NA ZIMAMOTO 1-0

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Zimamoto 1-0 kwenye mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Bao pekee la Yanga leo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa zamani wa JKU, Emmanuel Martin dakika ya 60 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Juma Mahadhi.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zake nne, sasa ikilingana na Singida United ambayo yenyewe iko juu kwa wastani wake mzuri wa mabao.
  Emmanuel Martin ameifungia Yanga bao pekee leo ikiilaza Zimamoto 1-0 Kombe la Mapinduzi 

  Yanga SC sasa watakutana na Singida United kesho Saa 2:15 usiku katika mchezo wa kuamua nani kinara wa kundi, mechi itakayotanguliwa na mchezo kati ya Simba SC na URA ya Uganda Saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan pia.
  Kikosi cha Zimamoto kilikuwa; Nassor Mrisho Salim, Yussuf Ramadhan Mtuba, Haji Nahodha Hajji, Suleiman Said Juma, Shaffi Hassan Rajab, Hassan Said Hassan, Hafidh Barik Juma/Hakim Khamis dk47, Khalid Kheir Mtwana, Uwezo Jeremiah Thomas/Nyange Othman Denge dk71, Ibrahim Hamad Ahmada na Hassan Haji Ali.
  Yanga SC; Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy/Raphael Daudi dk46, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent/Pato Ngonyani dk46, Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Yussuf Mhilu/Juma Mahadhi dk41, Papy Kabamba Tshishimbi/Ibrahim Ajib dk46, Matheo Anthony, Pius Buswita/Yohanna Nkomola dk57 na Emmanuel Martin.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDELEZA UBABE KOMBE LA MAPINDUZI, YAIZIMA NA ZIMAMOTO 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top