• HABARI MPYA

    Sunday, January 21, 2018

    WATFORD YAMTUPIA VIRAGO MARCO SILVA SABABU YA EVERTON

    Watford imemfukuza kocha Marco Silva baada ya Everton kuonyesha nia ya kumtaka PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    REKODI YA MATOKEO MABAYA YA WATFORD KWENYE LIGI KUU

    Leicester 2-0 Watford
    Watford 2-2 Southampton
    Manchester City 3-1 Watford
    Watford 1-2 Swansea
    Watford 2-1 Leicester 
    Brighton 1-0 Watford
    Watford 1-4 Huddersfield
    Crystal Palace 2-1 Watford
    Burnley 1-0 Watford
    Watford 1-1 Tottenham
    Watford 2-4 Manchester United 
    TIMU ya Watford imemfukuza kocha wake, Marco Silva na kuwalaumu Everton kwamba wamechangia wao kuwa na matokeo mabaya msimu huu.
    Kocha huyo Mreno aliipandizsha Watford hadi nafasi ya nane baada ya mechi 13 ikizidiwa pointi nne na timu ya nne kwenye msimamo wa ligi. 
    Lakini baada ya kukataliwa kwenda Everton, Watford imeshinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita za Ligi Kuu - matokeo mabaya zaidi kwa timu zilkizopo kwenye ligi - na kuifanya timu hiyo kuporomokea kwenye eneo la kushuka daraja.
    Wamiliki wa Watford, familia ya Pozzo imeshindwa kurejesha imani kwa Silva baada ya kutamkwa hadharani kwamba anatakiwa na mahasimu wao, Everton kufuatia kufukuzwa kwa Ronald Koeman Oktoba mwaka jana.
    Silva, aliyejiunga na Watford Mei mwaka jana baada ya kufanya kazi nzuri akiwa na Hull City, anakuwa meneja wa nane kufukmuzwa na familia ta Pozzo ndani ya miaka sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WATFORD YAMTUPIA VIRAGO MARCO SILVA SABABU YA EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top