• HABARI MPYA

  Monday, January 22, 2018

  NYOSSO ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMPIGA SHABIKI WA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
  BEKI wa Kagera Sugar, Juma Said Nyosso anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera baada ya kumpiga na kumuumiza shabiki wa Simbe jioni ya leo. 
  Walioshuhudia tukio hilo wanasema Nyosso alikerwa na shabiki huyo kushangilia mbele yake baada ya mechi timu yake ikichapwa 2-0 na Simba na wengine wanasema shabiki huyo alimtolea maneno ya kejeli beki huyo ‘asiye na masihara’.
  Shabiki huyo alianguka chini na kuonekana kama aliyepoteza fahamu na Polisi wakamkamata Nyosso na kuondoka naye. 
  Juma Nyosso akiwa mikononi mwa askari wa Jeshi la Polisi leo 
  Shabiki wa Simba aliyepigwa na Juma Nyosso akipatiwa huduma ya kwanza Uwanja wa Kaitaba

  Simba SC imewapa raha mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC irejee kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, ikifuatiwa na Azam FC pointi 30 na mabingwa watetezi, Yanga SC pointi 25.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao ya Simba leo, wazawa kiungo Said Hamisi Ndemla na mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco wote kipindi cha pili.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOSSO ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMPIGA SHABIKI WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top