• HABARI MPYA

  Monday, January 01, 2018

  MWENYEKITI YANGA AKIRI; “CHIRWA ANATUDAI FEDHA ZAKE ZA USAJILI”

  Na Abdallah Chaus, MWANZA
  KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amekiri mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa amegoma kushinikiza alipwe fedha zake za usajili.
  Akizungumza kwenye mkutano wa wanachama wa matawi mkoa wa mwanza uliofanyika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Nyamagana mjini Mwanza Ijumaa, Sanga amesema ni kweli Chirwa amegoma kwa sababu anadai kiasi cha fedha ambacho hakukiweka wazi.
  Yanga imeondoka leo hapa Mwanza moja kwa moja kwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, siku moja tu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa.
  Obrey Chirwa amegoma Yanga SC kushinikiza alipwe fedha zake za usajili

  Na kuhusu Chirwa, ambaye amerejea kwao, Zambia kushinikiza malipo yake, Sanga amesema;  “Hawa wachezaji tunaishi nao kama watoto wetu, tunafahamu na wenyewe ni binadamu kama sisi na wana maisha nje ya soka. Ni kweli tunadaiwa na Chirwa ila anatudai fedha za usajili pekee ambayo tulitakiwa kumlipa baada ya sisi kumsajli,”amesema.
  Lakini Sanga amekanusha madai kwamba kuna wachezaji wanadai mishahara, kwani wametumia zaidi ya Sh. Milioni 100 kulipa mishahara yote ya wachezaji hadi mwezi Novemba 2017 na sasa wanatayarisha mishahara ya Desemba.
  Sanga amewaomba wanachama wa Yanga watulia na kuacha kusikiliza maneno ya kwenye mitandao, badala yake wafanye kazi ya kuijenga klabu yao na waache malumbano.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI YANGA AKIRI; “CHIRWA ANATUDAI FEDHA ZAKE ZA USAJILI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top