• HABARI MPYA

  Wednesday, December 13, 2017

  TYSON FURY ARUHUSIWA KURUDI ULINGONI, AMTAKA JOSHUA

  BONDIA Tyson Fury ameruhusiwa kucheza ngumi za kulipwa baada ya kukubali adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni.
  Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani, amekuwa nje ya ulingo tangu amshinde Wladimir Klitschko Novemba mwaka 2015.
  Muingereza huyo alifungiwa Juni mwaka 2016 na taasisi ya Kupambana na Dawa za Kulevya Michezoni nchini Uingereza (UKAD), lakini sasa anaweza kuanza kucheza tena mwakani akikata leseni upya.
  Na baada ya kufutiwa adhabu hiyo, Fury mara mpja ameanza kumchokoza Muingereza mwenzake, anayeshikilia mataji ya WBA na IBF, Anthony Joshua.
  '@anthonyfjoshua uko wapi? Ninakuja kwako (sic) namba1 umwziba nafasi yangu sasa," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twiter.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY ARUHUSIWA KURUDI ULINGONI, AMTAKA JOSHUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top