• HABARI MPYA

  Tuesday, December 05, 2017

  OLIVER KUCHEZESHA MECHI YA MAHASIMU WA MANCHESTER JUMAPILI

  REFA Michael Oliver ameteuliwa kuchezesha mchezo wa ujao mahasimu wa Jiji la Manchester.
  Uwanja wa Old Trafford unatarajiwa kuhimili vishindo vya mpambano wa mahasimu, Manchester United na Manchester City Jumapili, moja kati ya mechi zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkali msimu huu.
  Timu hizo mbili kwa sasa zinafuatana juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku United wakionekana kama washindani kweli wa City kwenye mbio za ubingwa.
  Pointi nane zinazitenganisha kwa sasa timu hizo mbili bvaada ya mechi 15, na City haijaonja ladha ya kipigo msimu wote huu.

  Michael Oliver ameteuliwa kuchezesha mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Oliver atasaidiwa na washika vibendera Gary Beswick na Simon Bennett, wakati mezani atakuwapo Jon Moss. 
  Huu si mchezo wa kwanza wa mahasimu hao kwa mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyeibukia Ashington, kwani awali alichezesha mechi ya Machi timu hizo zilipokutana.
  Oliver ndiye aliyekataa penalti ya Marcus Rashford ambayo mashabiki wa Man United wanaamini ilikuwa ni halali.
  Katika mechi zilizotangulia za mahasimu hao, Oliver alimtoa kwa kadi nyekundu beki wa Man United, Chris Smalling timu hizo zilipokutana mwaka 2014.
  Mechi ya Jumapili Man United watamkosa kiungo wao, Paul Pogba aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Arsenal Uwanja wa Emirates baada ya kumchezea vibaya, Hector Bellerin.
  United imeamua kutokata rufaa, hivyo itakutana na kikosi cha Pep Guardiola bila mchezaji wake huyo ghali iliyemnunua kwa Pauni milioni 89.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OLIVER KUCHEZESHA MECHI YA MAHASIMU WA MANCHESTER JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top