• HABARI MPYA

  Monday, December 04, 2017

  MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCCO DIFAA YAUA 4-1

  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefunga bao moja, timu yake 
  Difaa Hassan El - Jadida ikishinda 4-1 dhidi ya Khouribga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan.
  Msuva, mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC alifunga bao lake dakika ya 71, likiwa la nne katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola.
  Simon Msuva (kulia) akimpongeza Hamid El Ahadad baada ya kufunga hat trick jana 

  Mabao mengine matatu ya DHJ yote yalifungwa na mshambuliaji chipukizi Mmorocco, Hamid El Ahadad dakika za 30, 40 na 57.
  Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida inafikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 19 za mechi 10.
  Kikosi Cha Difaa Hassan El Jadida Kilikuwa; Yahia El Filali, Youssef Aguerdoum/ Adil El Hasnaoui dk42, Marouane Hadhoudi, Bakary N’diaye, Anouar Jayid, Tarik Astati, Mohammed Ali Bemammer, Ayoub Nanah, Bilal El Magri/ Mario Bernard dk79, Hamid Ahadad/Chouaib El Maftoul dk73 na Saimon Msuva.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCCO DIFAA YAUA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top