• HABARI MPYA

  Wednesday, December 13, 2017

  MO IBRAHIM WA SIMBA AFIWA MWANAWE MDOGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Simba, Mohammed ‘MO’ Ibrahim amefiwa na mwanawe mdogo leo mjini Dar es Salaam.
  Taarifa hazijafafanu zaidi kuhusu msiba huo, lakini inaelezwa mtoto huyo mdogo amefariki katika hospitali ya Mwananyamala alipokuwa anapatiwa matibabu.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara ameongoza salamu za pole na rambirambi kwa mchezaji huyo kufuatia msiba huo.
  Mohammed ‘MO’ Ibrahim akiwa na mwanawe mdogo aliyefariki dunia leo mjini Dar es Salaam.

  “Pole sana kiungo wetu mnyumbufu @mohammedibrahim04 'MO' kwa kufiwa na mwanao mpendwa. Tumeumia sote kwa msiba huu wa mtoto wetu mdogo kabisa. Kwa niaba ya klabu ya @simbasctanzania pokea salaam zetu za pole kwa msiba huu mzito wewe na mama wa mtoto. Inna lillah wainna ilaihi Raajiun,”ameandika Manara katika ukurasa wake Instagram.
  Kiungo Said Hamisi Ndemla amekuwa mchezaji wa kwanza kuposti kumpa pole mchezaji mwenzake huyo wa Simba SC.
  Na Msiba huo umetokea jioni hii baada ya Mo Ibrahim kushiriki mazoezi kikamilifu na Simba SC leo uwanja wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam. Mungu aiweke peponi moja kwa moja roho ya malaika huyo. Amin.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MO IBRAHIM WA SIMBA AFIWA MWANAWE MDOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top