• HABARI MPYA

  Sunday, December 10, 2017

  KATIBU WA ZAMANI YANGA AFARIKI DUNIA, NI MZEE MISANGA ALIYEWAHI KUONGOZA TFF PIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEWAHI kuwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) enzi za FAT (Chama cha Soka Tanzania), Mohammed Misanga amefariki dunia leo akiwa ana umri wa miaka 72
  Misanga, Mbunge wa zamani wa jimbo la Singida Kusini (CCM), amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
  Misanga aliyezaliwa Macchi 15, mwaka 1945 amekuwa Mbunge wa Singida Kusini tangu mwaka 2010 na awali mbali ya kuwa kiongozi wa FAT alikuwa pia Katibu wa Yanga SC.
  Mohammed Misanga (kushoto) amefariki dunia leo akiwa ana umri wa miaka 72

  Misanga alikuwa Katibu mkuu wa Yanga wakati inaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kihistoria mwaka 1976 uliosababisha klabu kukatika vipande na baadaye kuzaliwa Pan Africa. 
  Na Misanga ndiye aliyetangaza kufukuza kwa wachezaji waandamizi wote wakiwemo akina Leodegar Tenga, Omar Kapera, Juma Pondamali, Mohamed ‘Adolf’ Rishard na wengineo.
  Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda Singida kwa mazishi yatakayofanyika Jumatano jioni.
  Mungu aipumzishe kwa amani roho ya marehemu. Amin.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KATIBU WA ZAMANI YANGA AFARIKI DUNIA, NI MZEE MISANGA ALIYEWAHI KUONGOZA TFF PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top