• HABARI MPYA

  Friday, December 16, 2016

  ITC YA ZULU YAFIKA, SASA KUICHEZEA YANGA KESHO NA WAJEDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE kiungo mpya wa Yanga, Justin Zulu kutoka Zambia yuko huru kuanza kuihezea timu yake kesho mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu baada ya Hati yake ya Uhamisho wake wa Kimataifa (ITC) kutumwa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jonas Kiwia ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba ITC ya Zulu imewasili pia.
  "ITC ya Zulu imefika, hivyo naye yuo hutu sasa kucheza Ligi Kuu,"alisems Kiwia.
  Justin Zulu (chini kushoto) yuko huru kuichezea Yanga kesho wa dhidi ya JKT Ruvu baada ya ITC yake kutumwa 

  Mapema jana, Kiwia alisema ITC za wachezaji wawili wapya wa kigeni wa Simba kutoka Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei nazo zimefika hivyo wako huru kuicheza timu yao Jumapili dhidi ya Ndanda FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITC YA ZULU YAFIKA, SASA KUICHEZEA YANGA KESHO NA WAJEDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top