• HABARI MPYA

    Monday, December 05, 2016

    GABRIELLE ABOUDI ONGUENE AWA MCHEZAJI BORA AWCON 2016

    KIUNGO wa Cameroon, Gabrielle Aboudi Onguene amekuwa Mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizofikia tamati Jumamosi nchini kwao.
    Lakini mabingwa, Nigeria wametoa mchezaji Bora ambaye ni Asisat Lamina Oshoala aliyefunga mabao sita nchini Cameroon, huku wenyeji wakishinda na tuzo ya Fair Play.
    Walioteuliwa kwenye kikosi cha AWCON ya mwaka huu, yaani 11 Bora kwa mtiririko wa nafasi uwnajani ni kipa; Annette Ngo Ndom (Cameroon), mabeki; Meffoumetou Tcheno Falone (Cameroon), Osinachi Ohale (Nigeria), Janine Van Wyk (Afrika Kusini) na Linda Eshun (Ghana) 
    Viungo ni Jermaine Seoposenwe (Afrika Kusini), Raisa Feudjio Tchuanyo (Cameroon), Elizabeth Addo (Ghana) na Gabrielle Aboudi Onguene (Cameroon) wakati washambuliaji ni Ugochi Desire Oparanozie (Nigeria) na Asisat Lamina Oshoala (Nigeria).
    Gabrielle Aboudi Onguene wa Cameroon ndiye mchezaji bora wa AWCON 2016

    Wachezaji wa akiba ni Alaba Jonathan (Nigeria), Marie Awona (Cameroon), Janet Egyir (Ghana), Francisa Ordega (Nigeria), Portia Boakye (Ghana) na Nothando Vilakazi (Afrika Kusini)
    Bao pekee la mshambuliaji Desire Oparanozie zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika, Jumamosi lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 Nigeria dhidi ya wenyeji Cameroon katika fainali ya AWCON Uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde.
    Oparanozie aliyefunga pia bao la ushindi katika Nusu Fainali dhidi ya Afrika Kusini siku nne zilizotangulia mjini Limbe, aliwanyamazisha mashabiki wa nyumbani wapatao 40,000 waliofurika uwanjani.
    Inakuwa mara ya tatu kwa Nigeria kuifunga Cameroon katika fainali baada ya mwaka 2004 na 2014.
    Na ushindi huo unaifanya Nigeria iwe nchi iliyotwaa mataji mengi ya AWCON bada ya awali kutwaa katika miaka ya 1998, 2000, 2002, 2002, 2006, 2010 na 2014.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GABRIELLE ABOUDI ONGUENE AWA MCHEZAJI BORA AWCON 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top