• HABARI MPYA

  Tuesday, August 03, 2021

  AZAM FC YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI CHAKE KWA KUMSAJILI KIPA NAMBA MOJA WA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR


  KLABU ya Azam FC imemsajili kipa Ahmed Ali Suleiman 'Salula' kutoka KMKM ya Zanzibarkwa mkataba wa miaka miwili.
  Golikipa huyo mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa saba Azam FC dirisha hili kuelekea msimu ujao na wa pili tu mzawa baada ya beki, Edward Charles Manyama kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.
  Wengine wote watano ni wageni, viungo, Mkenya Kenneth Muguna, Wazambia Paul Katema, Charles Zulu na washambuliaji Rodgers Kola na Mkongo Idris Mbombo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI CHAKE KWA KUMSAJILI KIPA NAMBA MOJA WA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top