• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 02, 2019

  AZAM FC WAREJEA LIGI KUU BARA NA HASIRA KAMA ZOTE, WAICHAPA NDANDA FC 2-0 CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imerudi kwa kishindo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamaz mjini Dar es Salaam.
  Ushindi wa Azam FC iliyo chini ya kocha Mrundi, Etienne Ndayiragije umetokana na mabao ya mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 32 na kiungo mzawa, Frank Domayo dakika ya 45.
  Na huo unakuwa ushindi wa pili tu katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu baada ya Agosti 27 kushinda 1-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam bao pekee la Iddi Suleiman ‘Nadio’.

  Azam FC walikuwa wanacheza mechi ya kwanza tangu watolewe kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na klabu ya Triangle ya Zimbabwe wakifungwa 1-0 nyumbani na ugenini katika Raundi ya Pili.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Donald Ngoma/Emmanuel Mvuyekure dk59, Daly Ella Richard D’jodi/Obrey Chirwa dk59 na Iddi Suleiman ‘Nado’/Joseph Mahundi dk74. 
  Ndanda FC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Aziz Sibo, Said Mbatty, Samuel Mauru, Paul Maona, Hemed Koja/Salumu Chubi dk52, Omary Issa, Omar Hassan, Hussein Javu/Munir Amaan dk83, Godfrey Malibiche na Kigi Makassy/Nasorro Hashim dk83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAREJEA LIGI KUU BARA NA HASIRA KAMA ZOTE, WAICHAPA NDANDA FC 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top