• HABARI MPYA

    Thursday, March 08, 2018

    NGORONGORO HEROES KUCHEZA NA MOROCCO MECHI YA KIRAFIKI DAR MACHI 17

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Morocco Machi 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
    Mchezo huo ni wa kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za Africa kwa Vijana dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaochezswa Machi 31, 2018.
    Morocco wanatarajia kutua Tanzania Machi 14,2018 ikiwa na msafara wa watu 31 wanaojumuisha wachezaji 23 na viongozi 8 wa benchi la ufundi. Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni.
    Said Mussa Bakari 'Side Ronaldo' (kushoto) wa Yanga amejumuishwa kikosi cha awali cha Serengeti Boys

    Kikosi cha Ngorongoro Heroes kimeingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya DRC kikiundwa na wachezaji 40 ambao watapunguzwa na kubaki wachezaji 30 baada ya wiki ya kwanza ya mazoezi. 
    Kikosi kilichoingia kambini; Ramadhan Kabwili(Yanga SC), Abutwalib Mshedi (Mtibwa Sugar), Johny Kwiyenda, Ally Salim (Simba), Kibwana Ally Shomari (Mtibwa Sugar), Ally Hussein Msengi, Enrick Vitalis Nkosi (African Lyon), Dickson Job (Mtibwa Sugar), Assad Juma (Singida United) na Said Mussa Bakari 'Side Ronaldo' (Yanga).
    Wengine ni Ally Ng’anzi (Singida United), Kelvin Nashon Naftal (JKT Tanzania), Shaaban Ada (Lipuli, Issa Makamba (Singida United), Mohamed Rashid (Singida United), Marko Gerald (JMK), Cyprian Mtesigwa (Dodoma FC), Muhsin Makame (Njombe Mji), Yohana Mkomola (Yanga SC) na Ibrahim Abdallah (Miembeni City).
    Wengine ni Abdul Suleiman (Ndanda FC), Nickson Kibabage (Njombe Mji), Mussa Najimu (Changanyikeni), Maziku Amani (Makongo), Hamisi Mustafa (Ndanda FC), Samson Myati (Toto Africans), Said Mohamed (Azam FC), Ayoub Mohamed (Yanga SC), Mohamed Mussa (Azam FC), Emanuel Myati(Tz Prisons) na Riffat Hamis(Mtibwa Sugar).
    Wamo pia Oscar Masai (Azam FC), Paul Peter (Azam FC), Vitalis Mayanga (African Lyon), Rajab Mohamed (Azam FC), Pontia Ohonya, Maka Anthony (Yanga SC), Israel Mwenda (Alliance), Hance Msonga (Alliance) na Moses Kitandu(Simba).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO HEROES KUCHEZA NA MOROCCO MECHI YA KIRAFIKI DAR MACHI 17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top