• HABARI MPYA

    Sunday, February 11, 2018

    MSUVA APIGA HAT TRICK, DIFAA YASHINDA 10-0 LIGI YA MABINGWA

    Na Mwandishi Wetu, EL JADIDA
    WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana amefunga mabao matatu, timu yake, Difaa Hassan El Jadida iksihinda 10-0 dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini Morocco.
    Msuva  aliye katikaa msimu wake wa kwanza klabu hiyo baada ya kujiunga nayo kutoka kwa mabingwa wa Tanzania, Yanga SC alifunga mabao yake katika dakika za 44, 72 na 88.
    Mabao mengine ya Difaa Hassan El Jadida yalifungwa na Bakary N'diaye dakika ya nne, Hamid Ahadad dakika za 23, 26, 37, 42 na 47 na Bilal El Magri dakika ya 54.
    Sasa akina Msuva watakwenda ugenini Guinea Buissau katika mchezo mwepesi kabisa baada ya ushinsi huo mnono wa nyumbani. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA APIGA HAT TRICK, DIFAA YASHINDA 10-0 LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top