MSHAMBULIAJI Harry Kane amesawazisha rekodi ya gwiji Steven Gerrard kutwaa tuzo sita za Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England baada ya kushinda na ya mwezi Desemba mwaka 2017.
Mchezaji huyo wa Tottenham amefunga mabao nane katika mechi sita, zikiwemo hat-tricks mbili mfululizo dhidi ya Burnley na Southampton katika mwezi wa mavuno.
Ameweka rekodi ya kufunga mabao 39 katika Ligi Kuu kwa mwaka na sasa anaungana na Nahodha wa zamani wa Liverpool katika vitabu vya historia.
Kane amesema kwamba alifurahi kupata tuzo hiyo wakati akijiandaa kurejea kwenye ligi kwa mchezo wa nyumbani kati ya Spurs na Everton wikiendi hii.
Gerrard alishinda tuzo ya kwanza ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu Machi 2001 na ya mwisho akatwaa miaka 13 baadaye.
Kane ameongoza katika orodha iliyokuwa na beki wa pembeni wa Chelsea, Marcos Alonso, Marko Arnautovic wa West Ham United, wachezaji wawili wa Liverpool, Roberto Firmino na Mohamed Salah, Jesse Lingard wa Manchester United, Riyad Mahrez wa Leicester City na beki wa Manchester City, Nicolas Otamendi.
0 comments:
Post a Comment