• HABARI MPYA

    Saturday, October 18, 2014

    PIGO TENA LIVERPOOL, STURRIDGE AUMIA TENA MAZOEZINI NA ATAKAA NJE WIKI TATU ZAIDI

    KLABU ya Liverpool imepata pigo kubwa jana wakati Daniel Sturridge alipotakiwa kuwa nje kwa angalau wiki tatu zaidi baada ya kuumia tena mazoezini.
    Kocha Brendan Rodgers amekuwa na matumaini kupona kwa mshambuliaji huyo kungeimarisha kikosi chake.
    Sasa Sturridge, ambaye aliumia ndama wakati wa kupasha misuli moto Melwood Alhamisi, atakosa mechi kadhaa ngumu zikiwemo za nyumbani na ugenini za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
    Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge anatarajiwa kuendelea kuwa nje kwa wiki tatu zaidi 

    MECHI ZA LIVERPOOL AMBAZO SASA STURRIDGE ATAZIKOSA

    1. QPR v Liverpool
    2. Liverpool v Real Madrid
    3. Liverpool v Hull
    4. Liverpool v Swansea
    5. Newcastle v Liverpool
    6. Real Madrid v Liverpool
    7. Liverpool v Chelsea
    Liverpool itakuwa na mechi saba katika wiki tatu zijazo ikiwemo ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Ligi, au Capital One dhidi ya Swansea Oktoba 28 na ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea Uwanja wa Anfield Novemba 8.
    Sturridge alipona maumivu ya mguu aliyopata akiichezea timu ya taifa ya England Septemba mwaka huu, maumivu ambayo yalizua mtafaruku baina ya Rodgers na kocha wa Three Lions, Roy Hodgson juu ya muda wa kupona kwa mpachika mabao huyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO TENA LIVERPOOL, STURRIDGE AUMIA TENA MAZOEZINI NA ATAKAA NJE WIKI TATU ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top