LIGI KUU ya England inaanza leo na Louis van Gaal anaanzisha rasmi zama mpya Manchester United atakapoiongoza dhidi ya Swansea City Uwanja wa Old Traffford.
Mwalimu huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda mechi tano na sare moja katika mech za kujiandaa na msimu na sasa watu wanataka kuangalia mafanikio yake katika ligi.
Swansea ni moja kati ya timu nane ambazo msimu uliopita zilishinda mechi Old Trafford Mashetani Wekundu wakiwa chini ya kocha David Moyes aliyetupiwa virago kwa matokeo mabaya mwishoni mwa msimu.
Ikumbukwe, United pia ilikutana na Swansea katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huo 2013-2014 wakiwa mabingwa watetezi na kushinda mabao 4-1 Uwanja wa Liberty, siku za mwanzoni za Moyes kazini.
Matokeo hayo hayakuwa na maana, kwani mwishoni mwa msimu United ilimaliza katika nafasi ya saba.
Wayne Rooney ataiongoza United kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Nahodha Jumanne timu hiyo ikishinda mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Valencia.
United itamkosa beki wake kinda wa kushoto mwenye umri wa miaka 19 iliyemnunua kwa Pauni Milioni 27, Luke Shaw, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama.
Baada ya kuimarisha kikosi kwa kusajili nyota kadhaa wapya, kocha Arsene Wenger ataiongoza Arsenal katika mchezo wa ugenini dhidi ya Crystal Palace.
Ikiwa imetoka kumaliza ukame wa miaka tisa wa mataji kwa kushinda Kombe la FA msimu uliopita, Arsenal ilifungua msimu vizuri kwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifumua Manchester City 3-0 wiki iliyopita.
Mchezaji mpya, Alexis Sanchez, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30 kutoka Barcelona, anatarajiwa kuwamo kwenye kikosi cha leo katika mchezo wa kwanza wa ushindani sambamba na Nahodha mpya, Mikel Arteta.
Palace inaingia katika mchezo wa leo ikiwa katika mgogoro, kufuatia taarifa za kuondoka kwa kocha Tony Pulis juzi baada ya kutofautiana na wamiliki juu ya sera ya usajili.
Mabingwa wa Championship, Leicester City watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda msimu huu, Queens Park Rangers itaikaribisha Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle United kesho.
Liverpool, iliyozidiwa kete na Man City katika mbio za ubingwa msimu uliopita, wataanza kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Lallana ataukosa mchezo huo kutokana na maumivu ya goti, lakini Lambert na Lovren wote wapo katika nafasi nzuri ya kuichezea Liverpool, ambayo imetoka kumuuza kinara wake wa mabao Luis Suarez kwa Barcelona.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc Fabregas itaifuata Burnley iliyoapanda msomu huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West Bromwich Albion na Sunderland na West Ham United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho Liverpool v Southampton, Newcastle United v Manchester City na keshokutwa Burnley v Chelsea.

![]() |
Kazi inaanza; Kocha Louis Van Gaal tayari kuanzisha zama mpya Manchester United leo |

Mabingwa; Manchester City wanaanza kutetea taji lao |
![]() |
Arsenal inaingia kwenye kampeni mpya na kikosi kilichoboreshwa |
![]() |
Kocha Jose Mourinho anaanza kujaribu tena kuipa ubingwa wa Chelsea |
Palace inaingia katika mchezo wa leo ikiwa katika mgogoro, kufuatia taarifa za kuondoka kwa kocha Tony Pulis juzi baada ya kutofautiana na wamiliki juu ya sera ya usajili.
Mabingwa wa Championship, Leicester City watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda msimu huu, Queens Park Rangers itaikaribisha Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle United kesho.
Liverpool, iliyozidiwa kete na Man City katika mbio za ubingwa msimu uliopita, wataanza kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Lallana ataukosa mchezo huo kutokana na maumivu ya goti, lakini Lambert na Lovren wote wapo katika nafasi nzuri ya kuichezea Liverpool, ambayo imetoka kumuuza kinara wake wa mabao Luis Suarez kwa Barcelona.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc Fabregas itaifuata Burnley iliyoapanda msomu huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West Bromwich Albion na Sunderland na West Ham United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho Liverpool v Southampton, Newcastle United v Manchester City na keshokutwa Burnley v Chelsea.
0 comments:
Post a Comment