• HABARI MPYA

    Sunday, May 24, 2026

    COASTAL UNION YAICHAPA MASHUJAA FC BAO 1-0 MKWAKWANI


    TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Bao pekee la Coastal Union limefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid Maulid dakika ya 66 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya 10 kutoka ya 13 wakiizidi pointi moja Mashujaa FC baada ya timu zote kucheza mechi 25 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA MASHUJAA FC BAO 1-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top