• HABARI MPYA

    Wednesday, August 13, 2014

    BEKI AIPA USHINDI APR KOMBE LA KAGAME, GOR MAHIA SASA HALI TETE

    BAO pekee la beki Emery Bayisenga (pichani chini) dakika ya 38, limeipa APR ushindi wa 1-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti katika mchezo wa Kundi B Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.
    APR inapanda kileleni mwa kundi hilo, kwa kufikisha pointi sita, sawa na KCC ya Uganda, lakini yenyewe ina wastani mzuri zaidi wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Bado tiketi ya Robo Fainali iko wazi kwa timu zote za kundi hilo kulingana na matokeo ya mechi zinazofuata yatakavyokuwa- kwani hata Gor Mahia ya Kenya inayoshika mkia ikiwa haina pointi, ikishinda mechi zake mbili zijazo itatimiza pointi sita. 

    Katika mchezo uliotangulia wa kundi hilo leo, bao pekee la Brian Umony pia, kwa penalti limeipa KCC ushindi wa 1-0 dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja huo huo.
    Mshambuliaji huyo aliyetemwa Azam FC mwishoni msimu, sasa anatimiza mabao mawili katika mashindano haya ndani ya mechi tatu na sasa anaingia kwenye mbio za ufungaji bora dhidi ya mshambuliaji wa timu yake ya zamani, John Bocco ‘Adebayor’.
    Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi A, Adama City ya Ethiopia na Atlabara ya Sudan Kusini na Rayon ya hapa dhidi ya KMKM ya Zanzibar, wakati Polisi ya hapa pia, itamenyana na vibonde Benadir ya Somalia katika mchezo wa Kundi C.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI AIPA USHINDI APR KOMBE LA KAGAME, GOR MAHIA SASA HALI TETE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top