• HABARI MPYA

    Thursday, August 14, 2014

    BASI LA TAIFA STARS LAKAMATWA KWA DENI LA SH MILIONI 140 LILILOACHWA NA TENGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BASI la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya Mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo tunadaiwa hadi litakapolipwa.
    Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. TFF imesema hadi sasa imekwishalipa Sh. Milioni 70 katika deni hilo. “Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo,”imesema taarifa ya TFF.
    Hili ndilo basi la Stars lililokamatwa kwa deni lililoachwa na utawala wa Tenga TFF

    Basi lililokamatwa ni ambalo TFF ilipewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars, aina ya Yutong na deni ni wakati ambao shirikisho hilo lipo chini ya Rais, Leodegar Tenga aliyemaliza muda wake mwaka jana. Kwa sasa, Rais wa TFF ni Jamal Malinzi aliyerithi deni hilo. 
    Mzee imekuwaje tena basi limekamatwa? Tenga ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CECAFA (kshoto) akiwa ni Mkurugenzi wa masoko wa TBL, Kushila Thomas (kulia)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BASI LA TAIFA STARS LAKAMATWA KWA DENI LA SH MILIONI 140 LILILOACHWA NA TENGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top