• HABARI MPYA

    Thursday, August 14, 2014

    ALLY BUSHIRI ANAHITAJI USHINDI TU DHIDI YA RAYON ILI KUBAKI KAGAME, VINGINEVYO ‘OUT’

    Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
    KOCHA Ally Bushiri ‘Bush’ anahitaji ushindi katika mchezo wake wake wa mwisho wa kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati leo dhidi ya wenyeji, Rayon Sport ili kuweka hai matumaini ya kubaki mjini Kigali, Rwanda.
    Baada ya kufungwa 4-0 na Azam FC ya Tanzania na kutoka sare za kufungana mabao 1-1 dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini na Adama ya Ethiopia, KMKM leo inatakiwa kuifunga Rayon Uwanja wa Nyamirambo kama inataka kwenda Robo Fainali.
    Safari imeiva? Kocha Ally Bushiri leo anatakiwa kuifunga Rayon ili kubaki Kigali 

    Japokuwa ilifungwa 4-0 na Azam FC, lakini timu hiyo ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo imeonyesha kuimarika siku hadi siku kadiri inavyoendelea na mashindano ya mwaka huu.
    Kocha Bush alisema kwamba KMKM ya sasa inaundwa na wachezaji wengi wapya na vijana wadogo ambao Kagame ya mwaka huu ndiyo mashindano yao ya kwanza kabisa.
    Amesema hiyo inafuatia kuisuka upya timu hiyo baada ya kuachana na wachezaji kadhaa wazoefu na kupandisha yosso.
    “Mwaka huu sikuja huku kwa matumaini, nimekuja ili vijana watoe woga, ila kwa kuwa tayari nina tiketi nyingine ya mashindano haya mwakani, vijana wangu watakuwa wapo tayari kabisa kushindana,”amesema Bush.  
    Mbali na KMKM kupepetana na Rayon leo, mchezo mwingine wa Kundi A utakuwa kati ya Adama City na Atlabara, wakati Polisi ya hapa pia, itamenyana na vibonde Benadir ya Somalia katika mchezo wa Kundi C.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALLY BUSHIRI ANAHITAJI USHINDI TU DHIDI YA RAYON ILI KUBAKI KAGAME, VINGINEVYO ‘OUT’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top