• HABARI MPYA

    Monday, February 03, 2014

    STRAIKA YANGA ALIYETIWA LUPANGO JANA AMEKWISHAACHIWA NA TAYARI YUPO KAMBINI

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    MSHAMBULIAJI Shaaban Kondo wa Yanga amejiunga na kikosi hicho cha Jangwani baada ya kuachiwa huru na waliomtia nguvuni jana.
    Baada ya mechi yao ya raundi ya 16 waliyoshinda 1-0 dhidi ya wababe Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana, kulitokea vurugu wakati askari walipomkunja na kumtia nguvuni mchezaji huyo wa Yanga aliyekuwa hajavaa sare pale alipokuwa akitaka kuingia katika vyumba vya kuvalia wachezaji wenzake. 
    Pole kijana; Shaaban Kondo kulia jana aliswekwa lupango

    Polisi walionekana kutomtambua kama ni mchezaji wa Yanga na akaondoka akiwa amebebwa kwenye gari la polisi.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu muda mfupi uliopita, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuto amaesema mchezaji wao huyo waliyemsajili msimu huu aliachiwa huru jana jioni baada ya uongozi kuzungumza na Jeshi la Polisi Kanda ya Temeke.
    "Mpaka sasa mchezaji wetu ameshaungana na wenzake, aliachiwa huru jana jioni," amesema Kizuguto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STRAIKA YANGA ALIYETIWA LUPANGO JANA AMEKWISHAACHIWA NA TAYARI YUPO KAMBINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top