• HABARI MPYA

    Saturday, February 08, 2014

    KASEJA WA KIMATAIFA AANZA LEO YANGA NA WACOMORO

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    MLINDA mlango Juma Kaseja leo ataidakia Yanga SC kwa mara ya kwanza katika mechi ya mashindano tangu asajiliwe dirisha dogo kama mchezaji huru, kufuatia kutemwa na Simba SC aliyoidakia kwa muda mrefu.
    Kaseja amepangwa katika kikosi cha kwanza kinachomenyana na Komorozine ya Comoro kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa ujumla hiyo itakuwa mechi ya sita kwa Kaseja kuidakia Yanga tangu arejee mwishoni mwa mwaka jana, baada ya awali kuidakia kwa msimu mmoja wa 2009.
    Mechi ya kwanza alidaka Yanga SC ikishinda 3-2 dhidi ya KMKM, ya pili Nani Mtani Jembe Yanga ikifungwa 3-1 na Simba SC, ya tatu katika sare ya 0-0 na KS Flamurtari Vlore, ya nne katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor na ya tano katika sare ya 
    2-2 na Simurq PIK, zote katika ziara ya Uturuki.
    Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza, Mrisho Ngassa na David Luhende.
    Anadaka leo; Juma Kaseja ataidakia Yanga mechi ya kwanza ya mashindano jioni hii

    REKODI YA KASEJA YANGA SC

    Yanga SC 3-2 KMKM (Kirafiki, alifungwa mbili Dar)
    Yanga 1-3 Simba SC (Mtani Jembe, alifungwa tatu Dar)
    Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki, hakufungwa)
    Yanga SC 3-0 Ankara Sekerspor (Ziara ya Uturuki, hakufungwa)
    Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki, alifungwa mbili)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEJA WA KIMATAIFA AANZA LEO YANGA NA WACOMORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top