| Wachezaji wa Azam FC wakishangilia ushindi wao wa leo wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. |
Mabao ya Azam leo yamefungwa na Brian Umony mawili dakika za 13 na 48, Kevin Friday dakika ya 51 na Jabir Aziz dakika ya 83.
Mbeya City ilikuwa timu nyingine ambayo haijafungwa, lakini leo rekodi hiyo imevunjwa na Yanga kwa kufungwa 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la Mrisho Ngassa dakika ya 16.
Matokeo ya leo yanaifanya Azam ijiimarishe kileleni kwa kutimiza pointi 36, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 34, ambayo pia imecheza mechi 16.
Mbeya City inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 31, moja zaidi ya Simba SC ambayo hata hivyo imecheza mechi 15.
Aidha, matokeo hayo yanamaanisha nafasi mbili za juu katika Ligi Kuu zinawaniwa na timu nne, ambazo ni Azam, Yanga, Mbeya City na Simba SC.


.png)
0 comments:
Post a Comment