• HABARI MPYA

    Friday, November 15, 2013

    YANGA YASAJILI KIUNGO CHIPUKIZI WA STARS KUTOKA RUVU SHOOTING


    Kifaa kipya; Hassan Saleh Dilunga amesaini miaka mitatu Yanga

    KLABU ya Young Africans Sports Club almaraafu kama Yanga imefanikiwa kumsaninisha mkataba wa miaka mitatu kiungo Hassan Saleh Dilunga kutoka timu ya Ruvu Shooting ambapo mchezaji huyo ataanza kuitumikia timu yake mpya katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
    Usajili wa kiungo Hassan Dilunga unakua ni usajili wa pili kwa klabu ya Young Africans katika kipindi cha dirisha dogo baada ya mwishoni mwa wiki kukamilisha kumsajili mlinda mlango Juma Kaseja.
    Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb amesema usajili wa kiungo huyo ni utekelezaji wa maagizo ya kocha mkuu Ernie Brandts aliyoyaacha pamoja na benchi lake la ufundi kwa ajili ya kuboresha kikosi.
    "Kocha aliacha mapendekezo ya usajili tuyafanyie kazi la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha tunampata Juma Kaseja kwa ajili ya kuongeza nguvu katika nafasi ya walinda mlango ambalo tulilikamilisha mwishoni mwa wiki na sasa tumelimaliza la kiungo Hassan Dilunga" alisema Bin Kleb.
    Kikubwa tunaendelea kuhakikisha kuwa maagizo yote yaliyopo katika ripoti ya benchi la ufundi tunyafanyia kazi na kuyatekeleza ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Klabu Bingwa Afrika. 
    IMEHAMISHWA KUTOKA TOVUTI YA YANGA SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YASAJILI KIUNGO CHIPUKIZI WA STARS KUTOKA RUVU SHOOTING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top