Na Mahmoud Zubeiry, Kariakoo
BEKI chipukizi wa Azam FC, Ismail Gambo maarufu kwa jina la utani, Kussi amesema kwamba watu wanamfananisha na Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Swedi ‘Kussi’, lakini hana uhusiano wowote na mlinzi huyo mkongwe wa Mtibwa Sugar.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, katika hoeli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam, Gambo alisema kwamba watu wamekuwa wakimuambia anafanana na beki huyo wa zamani wa Yanga kiasi cha kumpachika jina Kussi.
“Lakini siyo baba yangu kama watu wanavyosema, nafurahi tu kuitwa Kussi, kwa sababu nafananishwa na mmoja wa mabeki wazuri waliowahi kutokea katika nchi hii. Ila si baba yangu,”alisema.
Kussi ambaye yupo katika akademi ya Azam, alifanya vizuri katika timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars iliyoitwa kutafuta wachezaji wa kupandisha timu ya kwanza, Taifa Stars.
Bahati nzuri, Kussi amekuwa miongoni mwa wachezaji waliopandishwa Stars baada ya mechi dhidi ya Taifa Stars juzi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, timu ya pili ikishinda 1-0 bao pekee la Elias Maguri wa Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo, Kussi alionyesha uwezo mkubwa wa kuongoza safu ya ulinzi na kudhibiti washambuliaji kiasi cha kuwanyima nafasi wakali kama Mrisho Ngassa na Amri Kiemba kufunga hata bao la kuotea.
Alikuwa akishinda karibu kila mpira aliogombea na alikuwa akiwapanga vizuri wenzake katika kuzuia mashambulizi na kwa ujumla Kussi alionyesha ni hazina ya taifa.
Wachezaji walioitwa Stars ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo ‘Kussi’ (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Mourad (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Farid Mussa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Stars itamenyana na Kenya Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Baada ya hapo, Kim atateua kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kitakachokwenda, Kenya kwenye Kombe la CECAFA Challenge, michuano inayotarajiwa kuanza Novemba 27, mwaka huu mjini Nairobi.

![]() |
| Si baba yangu; Ismail Gambo 'Kussi' amesema hana uhusiano wowote na Salum Swedi 'Kussi' |
Kussi ambaye yupo katika akademi ya Azam, alifanya vizuri katika timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars iliyoitwa kutafuta wachezaji wa kupandisha timu ya kwanza, Taifa Stars.
Bahati nzuri, Kussi amekuwa miongoni mwa wachezaji waliopandishwa Stars baada ya mechi dhidi ya Taifa Stars juzi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, timu ya pili ikishinda 1-0 bao pekee la Elias Maguri wa Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo, Kussi alionyesha uwezo mkubwa wa kuongoza safu ya ulinzi na kudhibiti washambuliaji kiasi cha kuwanyima nafasi wakali kama Mrisho Ngassa na Amri Kiemba kufunga hata bao la kuotea.
![]() |
| Kussi mdogo na mkubwa; Salum Swedi kulia na Ismail Gambo kushoto, wote mabeki wa kati |
Alikuwa akishinda karibu kila mpira aliogombea na alikuwa akiwapanga vizuri wenzake katika kuzuia mashambulizi na kwa ujumla Kussi alionyesha ni hazina ya taifa.
Wachezaji walioitwa Stars ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo ‘Kussi’ (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Mourad (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Farid Mussa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
![]() |
| Kussi mdogo akimdhibiti Amri Kiemba |
![]() |
| Kussi mkubwa kulia akimdhibiti Mrundi Didier Kavumangu wa Yanga, hapa anaichezea Mtibwa anakomalizia soka yake hivi sasa |
![]() |
| Lishe bora; Kussi mdogo akipata chakula katika hoteli maarufu nchini, Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam ambako Future waliweka kambi |
Stars itamenyana na Kenya Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Baada ya hapo, Kim atateua kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kitakachokwenda, Kenya kwenye Kombe la CECAFA Challenge, michuano inayotarajiwa kuanza Novemba 27, mwaka huu mjini Nairobi.

.png)
0 comments:
Post a Comment