Na Princess Asia, Dar es Salaam
KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imewaruhusu wachezaji wake wawili nyota, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kurejea nchini Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya Jumanne ijayo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha TPM kimeondoka jana kwenda Accra, Ghana kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sfaxien ya Tunisia bila Samatta na Ulimwengu ambao watajiunga na timu hiyo kuanzia Jumatano.
Wachezaji wa kimataifa wa Zambia, Nathan Sinkala, Felix Sunzu na Hichani Himonde ambao waliichezea timu yao ikifungwa 2-0 na Misri jana, wanatarajiwa kujiunga na wenzao leo mjini Accra.
Mabingwa wa Afrika mara nne, Mazembe watamenyana na CS Sfaxien Jumamosi ya Novemba 23 mjini Tunis katika fainali ya kwanza ya CAF kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Lubumbashi, DRC.
Wachezaji walioitwa Stars ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo ‘Kussi’ (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Mourad (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Farid Mussa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

![]() |
| Mbwana Samatta anakuja |
![]() |
| Thomas Ulimwengu pia anakuja kuwavaa Kenya |

.png)
0 comments:
Post a Comment