Nyavu za magoli ya Uwanja wa Karume zimechakaa na zinapofugwa zinashikiziwa kwa mawe, kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa wachezaji. Mchezaji anaweza kuumia vibaya akiangukia kwa kishindo kikubwa moja ya mawe yaliyowekwa kwenye lango. Hii ni fedheha kwa nchi yetu, Uwanja huu ndio ambao timu zetu za taifa zinafanya mazoezi, lakini viongozi waliomaliza muda wao, chini ya Rais Leodegar Tenga hawakuliona hili na hawa walioingia madarakani chini ya Rais Jamal Malinzi pia hawajaliona hili. Je, wanasubiri siku mchezaji apasuliwe kichwa na mawe haya ndiyo wachukue hatua. Suti moja ya Tenga au Malinzi ingeweza kununua nyavu nzuri za kuweka kwenye magoli ya Karume na chenji wangerudishiwa, au na hili pia tunasubiri msaada wa FIFA?
Kipa Ivo Mapunda alihatarisha maisha yake jana angalia ma
we hayo chini
 |
| Suti moja tu ya Malinzi kulia au Tenga kushoto inaweza kununua nyavu nzuri Karume |
|
0 comments:
Post a Comment