• HABARI MPYA

    Thursday, November 14, 2013

    IVO MAPUNDA ASEMA YUKO TAYARI KUIDAKIA SIMBA SC, AWAKARIBISHA KWA MAZUNGUMZO

    Na Mahmoud Zubeiry, Ilala
    KIPA aliyerejeshwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya miaka mitano, Ivo Mapunda amesema Mkataba wake na Gor Mahia ya Kenya unaisha mwezi ujao hivyo Simba SC ambao wanatafuta kipa kama wameridhishwa na uwezo wake, anawakaribisha kwa mazungumzo.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya mechi ya jana baina ya Taifa Stars na timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars iliyoshinda 1-0, Ivo alisema kwamba milango iko wazi kwamba Simba SC kumfuata kwa mazungumzo.
    Ivo Mapunda akiwapungia mashabiki baada ya mechi jana

    “Ndiyo najua Simba SC wanatafuta kipa, mimi nasema kama wameridhishwa na uwezo wangu, waje tuzungumze na tukikubaliana nitawafanyia kazi nzuri,”alisema.
    Ivo aliidakia Stars kwa dakika 45 kipindi cha pili jana akimpokea Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyefungwa bao hilo la Elias Maguril aliyeunganisha pasi ya Juma Luizio 
    Mapema juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba wanatafuta kipa atakayekwenda kuwa pamoja na makipa wazawa, Abuu Hashimu na Andrew Ntalla, kwa kuwa wana mpango wa kuachana na kipa Mganda, Abbel Dhaira.
    Ivo akiokota taulo yake baada ya mechi



    Ivo akifurahia na Nadir Haroub 'Cannavaro'

    Bado imara; Ivo ameonyesha bado kipa mzuri

    “Niseme wazi, tunatafuta kipa. Huu ni mchakato makini sana na hatutaki kurudia kosa. Tunatafuta kipa mzawa, kwanza awe mwaminifu na mwenye uwezo mkubwa,”alisema.
    Ivo alikuwa kipa namba wa Tanzania wakati wa Marcio Maximo na tangu amejiunga na St George ya Ethiopia akitokea Yanga SC, hajawahi kuitwa tena Stars hata aliporejea nyumbani kuchezea African Lyon kabla ya kwenda Gor Mahia. 
    Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akifurahia na Ivo baada ya mechi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVO MAPUNDA ASEMA YUKO TAYARI KUIDAKIA SIMBA SC, AWAKARIBISHA KWA MAZUNGUMZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top