• HABARI MPYA

    Friday, November 15, 2013

    ROSTAM AZIZ NDIYE BABA WA MATAJIRI WOTE TANZANIA, MENGI WA PILI AFRIKA NZIMA KATIKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    TANZANIA imeongoza katika orodha ya tatu ya matajiri wapya wakubwa Afrika iliyotolewa na jarida la Forbes, mfanyabishara Rostam Aziz aliyeacha siasa kwa shinikizo la chama chake, CCM ili kubaki kwenye biashara pekee akitajwa kuwa tajiri zaidi nchini.
    Rostam aliyejiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011, jarida la Forbes limesema ana utajiri wa thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 1. 
    Mtanzania tajiri zaidi; Rostam Aziz ana zaidi ya dola Bilioni 1

    Rasilimali zake kubwa ni pamoja asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya Vodacom Tanzania, kampuni kubwa ya simu za mkononi Tanzania, ikiwa na wateja zaidi ya milioni 9.5; kampuni ya madini ya Caspian Mining, pamoja na biashara anazofanya kwa kushirikiana na  na bilionea wa Hong Kong, Li Ka-shing. Azizi pia amewekeza Dubai na Oman.
    Mtanzania mwingine, Reginald Mengi ni tajiri mkubwa wa pili Afrika katika uwekezaji kwenye sekta ya Habari, baada ya Koos Bekker wa Afrika Kusini. Binafsi, Mengi anamiliki kampuni ya IPP yenye magazeti 11, Televisheni tatu na vituo 10 vya Redio. 
    Rasilimali nyingine za Mengi ni migodi ya dhahabu, kampuni kadha za madini na kampuni ya soda ya Coca-Cola. Ana utajiri wa jumla ya dola za Kimarekani Milioni 550 kwa mujibu wa tathmini za FORBES.
    Mtu mpya katika orodha ya matajiri 50 wa Forbes 50 ni Mualgeria, Issad Rebrab, ambaye ameingia na tajiri wa thamani ya dola Milioni 3.2. Rebrab ni muanzilishi wa Cevital, kampuni ya familia inayotengeneza sukari, mafuta ya kupikia na jibini. Cevital pia inamiliki viwanda vya uzalishaji bidhaa za kusambaza.
    Bilionea wa Kenya na Afrika Mashariki, Vimal Shah ameingia kwenye orodha hiyo na utajiri wake wa dola Bilioni 1.6. Shah, baba yake na kaka yake kwa pamoja wanamiliki kampuni ya mafuta ya kupikia Bidco. 
    Pato la mwaka la kampuni hiyo ni dola Mlioni 500. Bidco pia inatengeneza unga wa chakula na sabuni za manukato katika nchi 14 Afrika. Pia ni muwekezaji wa Tatu City, kampuni mpya yenye thamani ya dola Bilioni 3  ya Satellite itakayokuwa na maskani yake, Nairobi.
    Mmorocco, Aziz Akhannouch ana utajiri wa dola Bilioni 1.4 kutokana na kumiliki kwake kampuni ya Akwa Group, iliyoanzishwa na baba yake ambayo kwa sasa inamiliki kampuni za Afriquia Gas na Maghreb Oxygene pamoja na vyombo vya habari, uwekezaji wa ardhi na hoteli. Akhannouch kwa sasa ni Waziri wa Kilimo na Uvuvi wa Morocco. Mkewe, Salwa Idrissi, anamiliki majengo ya kifahari.
    Aspen Pharmacare, walioshiriki kuanzisha Gus Attridge ya Afrika Kusini wameingia kwenye orodha hiyo kwa utajiri wao wa dola Milioni 525.
    Mtanzania, Mohammed ‘Mo’ Dewji anaingia katika orodha hiyo kwa utajiri wake wenye thamani ya dola milioni 500. Ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya METL, iliyoasisiwa na baba yake, Gulam Dewji. Baada ya kumaliza masomo ya biashara katika chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani alirejea nyumbani kuendeleza biashara za baba yake na pia kwa sasa ni mwanasiasa, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini.




    RankNameNet WorthAge
    1

    Aliko Dangote

    $20,800 M56
    2

    Johann Rupert & family

    $7,900 M63
    3

    Nicky Oppenheimer & family

    $6,600 M68
    4

    Nassef Sawiris

    $5,900 M52
    5

    Mike Adenuga

    $4,600 M60
    6

    Christoffel Wiese

    $3,800 M72
    7

    Isabel dos Santos

    $3,500 M40
    8

    Issad Rebrab

    $3,200 M69
    9

    Mohamed Mansour

    $3,100 M65
    10

    Othman Benjelloun

    $2,800 M81




    RankNameNet WorthAge
    11

    Patrice Motsepe

    $2,700 M51
    11

    Naguib Sawiris

    $2,700 M59
    13

    Folorunsho Alakija

    $2,500 M62
    14

    Yasseen Mansour

    $2,400 M52
    15

    Youssef Mansour

    $2,300 M68
    16

    Onsi Sawiris

    $2,000 M83
    17

    Miloud Chaabi

    $1,900 M84
    18

    Vimal Shah & family

    $1,600 M53
    19

    Stephen Saad

    $1,500 M49
    20

    Aziz Akhannouch & family

    $1,400 M52




    RankNameNet WorthAge
    20

    Desmond Sacco

    $1,400 M71
    22

    Anas Sefrioui

    $1,300 M56
    23

    Abdulsamad Rabiu

    $1,200 M53
    24

    Koos Bekker

    $1,100 M60
    24

    Sudhir Ruparelia

    $1,100 M57
    24

    Samih Sawiris

    $1,100 M56
    27

    Rostam Azizi

    $1,000 M49
    28

    Jim Ovia

    $900 M59
    29

    Theophilus Danjuma

    $700 M74
    29

    Cyril Ramaphosa

    $700 M60




    RankNameNet WorthAge
    31

    Lauritz (Laurie) Dippenaar

    $650 M65
    32

    Strive Masiyiwa

    $600 M52
    33

    Oba Otudeko

    $575 M69
    34

    Hakeem Belo-Osagie

    $550 M58
    34

    Mohammed Indimi

    $550 M65
    34

    Reginald Mengi

    $550 M-
    37

    Gus Attridge

    $525 M52
    38

    Raymond Ackerman

    $500 M82
    38

    Said Salim Bakhresa

    $500 M64
    38

    Sani Bello

    $500 M70





    RankNameNet WorthAge
    38

    Mohammed Dewji

    $500 M38
    38

    Moulay Hafid Elalamy

    $500 M53
    43

    Gerrit Thomas (GT) Ferreira

    $475 M65
    43

    Jannie Mouton

    $475 M66
    45

    Adrian Gore

    $460 M49
    46

    Shafik Gabr

    $450 M61
    46

    Alami Lazraq

    $450 M63
    48

    Naushad Merali

    $430 M62
    49

    Femi Otedola

    $410 M47
    50

    Tunde Folawiyo

    $400 M53
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROSTAM AZIZ NDIYE BABA WA MATAJIRI WOTE TANZANIA, MENGI WA PILI AFRIKA NZIMA KATIKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top