• HABARI MPYA

    Friday, November 15, 2013

    OLIECH NA HARAMBEE STARS KUFIKISHIWA USWAHILINI KIGOGO MBURAHATI

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    KENYA inakuja kucheza na Tanzania, Taifa Stars Jumanne katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na tayari Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limeipatia hoteli ya kufikia timu hiyo.
    Habari za ndani kutoka TFF ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zinasema kwamba Kenya inayokuja na nyota wake wa Ulaya, akiwemo Dennis Oliech anayecheza Ufaransa itafikia katika hoteli moja iliyopo Kigogo Mburahati, Dar es Salaam.
    Kutoka Ufaransa hadi Kigogo Mburahati kwenye 'vigodoro'; Dennis Oliech wa Harambee Stars

    Mchezo huo utakafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni maalum kwa kocha Kim Poulsen kujua ubora wa wachezaji wake, baada ya kuunda upya kikosi chake, kufuatia timu hiyo kukosa tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil.   
    Mdenmark huyo aliunda vikosi viwili, Future Young Taifa Stars na Taifa Stars ambavyo vilimenyana Jumatano Uwanja wa Karume Dar es Salaam. Future walishinda 1-0, bao pekee la Elias Maguri.
    Baada ya hapo akachukua wachezaji 16 kutoka kila kikosi kuunda kikosi cha wachezaji 32 walioingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Harambee.
    Walioitwa Stars ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo ‘Kussi’ (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Mourad (Azam).
    Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
    Viungo washambuliaji ni Farid Mussa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
    Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OLIECH NA HARAMBEE STARS KUFIKISHIWA USWAHILINI KIGOGO MBURAHATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top