• HABARI MPYA

    Friday, November 15, 2013

    MOURAD: SIKUTARAJIA KABISA KUITWA STARS BAADA YA SURE BOY ‘KUNIVUNJA’ KARUME

    Na Mahmoud Zubeiry, Ilala
    BEKI wa kati wa Azam FC, Said Mourad ‘Mweda’ amesema kwamba hakutarajia kabisa kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kuumia kifundo cha mguu Jumatano akiichezea timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars dhidi ya timu hiyo ya kwanza.
    Mourad aliumia kipindi cha kwanza na kutoka nje, ambako alifungwa bandeji na barafu kutokana na maumivu makali.
    “Nimeumia kifundo cha mguu, kanigonga Sure Boy (Salum Abubakar wa Azam pia aliyechezea Taifa Stars), ilikuwa bahati mbaya tu nimeweka mguu kapiga, nikaumia kwa sababu viatu vyake ni vigumu sana,”alisema Mourad baada ya mechi hiyo juzi, ambayo Future ilishinda 1-0.
    Sikutarajia; Said Mourad baada ya kuumizwa na Sure Boy juzi Karume

    Mourad amesema anamshukuru Mungu kwa kuitwa Taifa Stars na anazidi kumuomba aendelee kufanikiwa katika timu hiyo kwa sababu anaamini uwezo anao.
    “Watu wengi wanasema mimi ni kati ya mabeki wachache bora katika nchi hii, suala ni bahati tu, lakini uwezo ulikwishaonekana siku nyingi tu tangu enzi za Maximo (Marcio, Mbrazil aliyekuwa kocha wa Stars), bahati tu ya kupewa nafasi na kuaminiwa ndiyo nayoililia kwa sasa,”alisema.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen janalitaja wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
    Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo ‘Kussi’ (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Mourad (Azam).
    Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
    Viungo washambuliaji ni Farid Mussa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
    Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOURAD: SIKUTARAJIA KABISA KUITWA STARS BAADA YA SURE BOY ‘KUNIVUNJA’ KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top