• HABARI MPYA

    Sunday, November 17, 2013

    INIESTA AOTA MBAWA MAN UNITED, AAMUA KUBAKI BARCA

    KLABU ya Manchester United imepata pigo kubwa baada ya nyota wa Barcelona iliyekuwa inamtaka, Andres Iniesta kukubali kusaini Mkataba mpya na klabu yake hiyo ya Hispania.
    Mkurugenzi wa Michezo wa Barca, Andoni Zubizarreta amesema kiungo huyo yuko karibu kusaini Mkataba mpya na vinara hao wa La Liga.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ilielezwa hafurahii maisha Nou Camp kutokana na kutofautiana na mabosi wa timu hiyo, hivyo kumpa matumaini kocha David Moyes, ambaye amekuwa akimmezea mate na kutaka kumsajili Januari. 
    Pamoja na hayo, kipa wa zamani wa Barca, Zubizarreta amepuuza madai kwamba Iniesta ataihama klabu hiyo.
    Anabaki? Andres Iniesta ilielezwa hafurahii maisha Barcelona, lakini sasa imeelezwa atasaini Mkataba mpya Blow: Manchester United manager David Moyes (above) was said to be planning a bid for Iniesta in January
    Pigo: Kocha wa Manchester United, David Moyes (juu) ilielezwa anataka kumsajili Iniesta Januari
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: INIESTA AOTA MBAWA MAN UNITED, AAMUA KUBAKI BARCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top