• HABARI MPYA

    Sunday, November 17, 2013

    CAMEROON YAIFUMUA TUNISIA 4-1 NA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014, ETO’O…

    Na Princess Asia, Younde
    TIMU ya taifa ya Cameroon imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuifumua kwa mabao 4-1 Tunisia jioni ya leo kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde, Cameroon.
    Mabao ya Pierre Webo dakika ya nne, Benjamin Moukandjo dakika ya 30 na mawili ya Jean Makoun dakika za 66 na 86 yametosha kuwahakikishia Simba Wasiofungika kucheza fainali hizo kwa mara ya saba. 
    Jean Makoun amefunga mawili

    Bao pekee la Tunisia lilifungwa na Ahmed Akaichi dakika ya 50. Kocha wa Cameroon, Volker Finke alifanya mabadiliko matatu katika kikosi chake kutoka kile kilichotoa sare ya bila kufungana na Tunisia katika mchezo wa kwanza.
    Bennoit Assou-Ekotto, Stephane Mbia na Benjamin Moukandjo walianza kwenye kikosi cha kwanza badala ya Nyom, Nounkeu na Joel Matip. Samuel Eto’o alianza katika safu ya ushambuiaji pamoja na mkongwe Pierre Webo.
    Ruud Krol, naye kwa upande wake alibadilisha wachezaji wawili baada ya kushindwa kupata bao mjini Rades mwezi uliopita. Karim Haggui na Fakhreddine Ben Youssef walichukua nafasi za Sami Allagui na Alaeddine Yahia.
    Cameroon sasa inaungana na Nigeria na Ivory Coast kujihakikishia nafasi ya kwenda Brazil mwakani.
    Kikosi cha Cameroon kilikuwa: Itandje; Nkoulou, Chedjou, Mbia/Nounkeu dk70, Assou-Ekotto, Song, Makoun, Enoh, Moukandjo/Nguemo dk83, Webo/Choupo-Moting dk63 na Eto’o.
    Tunisia: Chrifia; Derbali, Mikari, Haggui, Benyoussef, Ragued, Yahya/Allagui dk74, Chikhaoui/Camus dk46, Ben Youssef, Chermiti/Akaichi dk46 na Khalifa.Qualified: Samuel Eto'o's (in action in the first leg) Cameroon are through to the World Cup after beating Tunisia
    Samuel Eto'o's akipambana na mchezaji wa Tunisia leo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAMEROON YAIFUMUA TUNISIA 4-1 NA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014, ETO’O… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top