KAKA yake Lionel Messi amejitoa mzima mzima kumpigia kampeni nyota wa Barcelona kuelekea tuzo za Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d’Or.
Huku zoezi la upiga kura likiwa njiani kwa tuzo hiyo ya FIFA, Matias Messi ametweet picha ya tuzo za kaka yake alizotwaa tangu mwaka 2009 sambamba na za mpinzani wake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa kipindi hichi.
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Frank Ribery naye anapewa nafasi kubwa pia kuwapiga bao Messi na Ronaldo pamoja na nyota wa Paris-Saint Germain, Zlatan Ibrahimovic aliye kwenye mbio hizo.
Ghala la tuzo: Kaka yake Lionel Messi, Matias ametweet picha hii kutia chachandu mjadala wa Ballon d'Or na mchoro (chini) unalinganisha baina ya nyota huyo wa Barcelona na Cristiano Ronaldo nani ana tuzo nyingi
Wakati huo huo, Messi atatumia muda wote Desemba kutulia Argentina akijaribu kutafuta ahueni na awe fiti kabisa kuitumikia Barcelona.
Klabu hiyo imetangaza wiki hii kwamba hatacheza tena hadi Januari 12. Habari zinasema kwamba mshindi huyo wa tuzo ya dunia mara nne, ameathiriwa na safari nyingi akiwa amesafiri umbali wa kilimota 120,000 ndani ya siku 64 kuzunguka nchi mbalimbali.



.png)
0 comments:
Post a Comment