• HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2018

    TFF YAMPA ULAJI AMMY NINJE, SASA KOCHA MKUU TIMU YA TAIFA YA VIJANA U-20

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA kocha wa Kilimanjaro Stars katika Challenge mwaka jana, Ammy Ninje ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
    Ngorongoro Heroes inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana (AFCON U20).
    Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Ammy Ninje ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa Ngorongoro Heroes 

    Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshasa, DRC.
    Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.
    Ninje anapewa Ngorongoro baada ya kuweka rekodi mbaya kwenye Challenge nchini Kenya mwaka jana, Kili Stars ikiondoka bila kushinda hata mechi moja, ikiambulia sare moja na kufungwa mechi zote.
    Katika michuano hiyo, pamoja na Ninje kuboronga, aliwakera Watanzania kwa majibu yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAMPA ULAJI AMMY NINJE, SASA KOCHA MKUU TIMU YA TAIFA YA VIJANA U-20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top