• HABARI MPYA

    Friday, March 16, 2018

    KAKOLANYA ALIYEPOTEZA NAFASI YANGA HUENDA AKAIBUKIA JKT TANZANIA AU KMC MSIMU UJAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA wa Yanga,  Beno Kakolanya ameingia ameingia katika rada ya JKT Tanzania na KMC FC  kwa ya kuhutaji huduma yake kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
    Kakolanya ni kipa namba tatu ndani ya kikosi cha Yanga, tayari ameshaingia sokoni baada ya mkataba wake kumalizika Julai Mwaka huu.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo mjini Dar es Salaam, Meneja wa kipa huyo, Suleiman Haroub amesema kwamba hadi sasa amepokea ofa nne ikiwemo za timu JKT Tanzania  na KMC.
    Alisema mbali na timu hizo mbili zilizomfuata na kutaka mazungumzo, lakini kwa sasa anaipa kipaumbele timu yake ya sasa, Yanga SC.
    Benno Kakolanya amepoteza uaminifu mbele ya benchi la Ufundi la Yanga na sasa hana nafasi tena kikosini

    "Ni kweli hizo offa zipo, wamekuja tumezungumza nao, pia nawasikilizia Yanga ambao hadi sasa wapo kimya,'alisema.
    Haroub alisema licha za timu hizo, pia milango ipo wazi kwa timu nyingine zinazohitaji huduma ya mchezaji huyo.
    Kakolanya ameachwa hapa nchini akiendalea kujifua kivyake wakati Yanga imekwenda Bostwana kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers kesho.
    Yanga inahitaji ushindi wa ugenini wa mabao 2-0 baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
    Kakolanya amepoteza nafasi Yanga mbele ya Mcameroon, Youthe Rostand na kinda mzawa, Ramadhani Kabwili wanaopokezana kudaka kwa sasa kutokana na kujivunjia uaminifu mbele ya benchi la Ufundi kwa kufanya mgomo kushinikiza apewe mkataba mpya.
    Kwa kugoma, benchi la Ufundi la Yanga chini ya kocha Mzambia, George Lwandamina limeona bora kuachana naye na kuamua kuendelea kufanya kazi na Rostand na Kabwili pekee. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAKOLANYA ALIYEPOTEZA NAFASI YANGA HUENDA AKAIBUKIA JKT TANZANIA AU KMC MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top