• HABARI MPYA

    Friday, March 16, 2018

    CHUKUA HIYO; WATU KIBAO WANAFANYA KAZI KWA KUJITOLEA TFF AKIWEMO AFISA HABARI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema wafanyakazi wake wengi kwa sasa wanafanya kazi kwa kujitolea, akiwemo Afisa Habari, Clifford Ndimbo.
    Katika taarifa maalum ya kujibu shituma za Makamu wake wa Rais iliyemfungia maisha, Michael Wambura, TFF imesema; "TFF haijawahi kuajiri mfanyakazi zaidi ya mmoja kwenye nafasi moja,wengi waliokuwepo kwenye Shirikisho kwa sasa wanajitolea akiwemo Afisa Habari,".
    Jana, Kamati ya Maadili ya TFF ilitangaza kumfungia maisha Wambura kutojihusisha na masuala ya soka kwa makosa matatu kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013. 
    Hiyo ni baada ya kikao chake cha juzi kufuatia Wambura kufikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.
    Rais wa TFF, Wallace Karia akitafakari mambo hivi karibuni mjini Dar es Salaam 

    Akizungumzia hatua hiyo jana, Wambura alisema kwamba Kamati iliyomfungia haina mamlaka, kwa sababu yeye anawajibika kwenye Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu.
    Wambura amesema kwamba kwa sasa anasubiri barua rasmi kutoka kwenye Kamati hiyo ili kuchukua hatua rasmi. 
    Wambura amesema mara baada ya kufungiwa kwamba kamati hiyo haina mamlaka ya kufanya, hivyo anawajibika kwenye kamati ya utendaji na Mkutano Mkuu.
    Alisema anasubiri barua rasmi ili kutoa maamuzi juu ya kusimamishwa huko.
    Wambura alisema suala la kujilipa fedha kupitia, JECK SYSTEM LIMITED ni suala la muda mrefu sana na lipo chini ya TAKUKURU.
    "Hili jambo hilo limepangwa kimikakati na sio suala la kisheria, kwani hapo kuna mambo matatu, ajira za TFF, Fedha na Makamu,"alisema.
    Wambura alisema katika suala la ajira ni baada ya kuleta hoja juu ya nafasi ya katibu mkuu kuhutaji wa kuajiriwa.
    "Ukiangalia nafasi ya Katibu anatakiwa kutangaza pia, haruhusiwi kupewa kama yupo moja ya kamati ya utendaji, kama ilivyo  wa sasa anacheo katika Chama cha makocha, " alisema. 
    Wambura alisema suala la fedha ni baada ya kuwa katika nafasi ya uenyekiti ya kamati ya fedha,  akibaini mambo mengi juu ya matumizi.
    "Ukiangalia matumizi ya miezi sita ni billioni 3 na hakuna tulichokifanya," alisema.
    Alisema kwa hali hiyo atapambana na hizo njama kuhakikishia hatashindwa.
    Na baada ya tuhuma hizo, TFF sasa wakajibu kwa taarifa hii; 
    1.Matumizi mabaya ya fedha za TFF
    JIBU : Wambura kama Mwenyekiti wa kamati ya fedha amehudhuria vikao zaidi ya 4 vya kamati na hajawahi kulalamika kokote mpaka amefungiwa.
    Bajeti ya TFF iliyopitishwa Dodoma kwa Mwaka Mzima ni Bilioni 8.6 hivyo matumizi anayosema ya Bilioni 3 kwa miezi 7 yanaonyesha jinsi gani TFF inavyopambana na changamoto za kifedha hivyo kuhakikisha inapunguza matumizi.
    Mapato yaliyopatikana kwa miezi Saba(7) iliyopita yalitumika katika maeneo yafuatayo :
    Timu ya Taifa Taifa stars(Fifa dates),Kilimanjaro Stars  (Challange Cup),Kambi kwa Timu ya Taifa Under23,Kambi U20,U16,Wanawake U20,Ligi za Wanawake,Kombe la Shirikisho la Azam,kozi za makocha,kozi za waamuzi za nje na ndani,vikao vya kamati ya utendaji na  kamati ndogo ndogo,mishahara ya watumishi wa TFF na makocha wa timu za Taifa,kulipa madeni tuliyoyakuta na kuidhinishwa na kamati ya fedha,kozi za Grassroots na Live Your Goal na soka la Ufukweni
    2.Ajira za TFF watu kupewa kwa kujuana.
    JIBU : TFF haijawahi kuajiri nafasi yoyote ile zaidi ya Wakurugenzi 3 na meneja 1 tofauti na uongo unaozungumzwa,Wakurugenzi walioajiriwa ni Mkurugenzi wa Fedha,Mkurugenzi wa Mashindano,Mkurugenzi wa sheria na Wanachama na Meneja Masoko,katika kupunguza matumizi ya fedha Taasisi imebaki na Wafanyakazi 21 kutoka 44 wa awali waliokutwa na Ndugu Karia.
    3.Kumteua Wilfred Kidao kuwa kaimu Katibu Mkuu wa TFF.
    JIBU : Kaimu Katibu Mkuu alikaimishwa na Kamati ya Utendaji na yeye Wambura akiwa mmoja wa waliompitisha.
    4.Mipira 100 kila mkoa kwamba kuna watu wamepiga fedha za TFF.
    JIBU : TFF chini ya Rais wa TFF aliyekuwepo madarakani Ndugu Wallace Karia haijawahi kununua mipira,mipira iliyotolewa ilinunuliwa na uongozi uliopita ilichofanya TFF ni kuigawa kama ilivyofanya.
    5.Kuwa na wafanyakazi wawili kwenye nafasi moja.
    JIBU : TFF haijawahi kuajiri mfanyakazi zaidi ya mmoja kwenye nafasi moja,wengi waliokuwepo kwenye Shirikisho kwa sasa wanajitolea akiwemo Afisa Habari.
    6.Suala la Waamuzi kuondolewa kuchezesha ligi kuu.
    JIBU : Ili kuongeza ubora wa uchezeshaji TFF ikaamua kuchaguwa waamuzi wa juu(Elite) tofauti na awali ambako kulikuwa na idadi kubwa mchanganyiko ya waamuzi.
    7.Kaimu Katibu kutuma majina ya Makamishina.
    JIBU : Jina la Michael Wambura na Ahmed Mgoyi ndio yaliyopelekwa kama utaratibu unavyotaka ya kujaza kwenye fomu moja pekee na TFF haikuwahi kubadilisha wala kukata jina la mtu yeyote.
    8.TFF ya sasa mpaka uwe na urafiki na watu 3 Karia, Mgoyi, na Nyamlani.
    JIBU : TFF haiendeshwi kwa urafiki bali kwa utaratibu wenye kufuata kanuni.
    Kikao kilichotoa maamuzi ni Kamati inayojitegemea(Independent) sio rahisi kuingiliwa kwakuwa hata Rais wa TFF hawezi kuiingilia
    Kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaoenezwa kwa maslahi binafsi,ni vyema watu wakajikita kwenye kujibu tuhuma zao bila kuhusisha uongo na vitu visivyo vya kweli kwa Taasisi ambayo kwasasa ipo makini kwenye kuhakikisha kila kitu kinafuata utaratibu ikiwemo masuala ya kifedha pamoja na mambo mengine.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHUKUA HIYO; WATU KIBAO WANAFANYA KAZI KWA KUJITOLEA TFF AKIWEMO AFISA HABARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top