• HABARI MPYA

  Saturday, February 03, 2018

  SINGIDA UNITED WANG’ARA NAMFUA, WAICHAPA 3-2 MWADUI FC

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Namfua, Singida. 
  Ushindi huo, unaifanya Singida United ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ifikishe pointi 30 baada ya kucheza mechi 16 na kupanda hadi nafasi ya tatu wakiwashushia mabingwa watetezi, Yanga SC katika nafasi ya nne.
  Lakini Yanga SC iko uwanjani hivi sasa inacheza mechi yake ya 16 dhidi ya wenyeji, Lipuli ya Iringa Uwanja wa Samora na ikishinda itarudi nafasi ya tatu.
  Haukuwa ushindi mwepesi kwa Singida United hivi leo, kwani Ilibidi watoke nyuma kwa mabao 2-0 ili kubeba pointI zote za mchezo wa leo.
  Kenny Ally Mwambungu baada ya kufunga bao la tatu na la ushindi kwa Singida dakika ya mwisho leo
   
  Mwadui FC ilitanguliwa kwa mabao ya viungo wake mahiri, mkongwe Awadh Juma dakika ya 11 na Awesu Awesu dakika ya 31.
  Hata kabla ya filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza Singida United walikomboa mabao yote mawili, Salum Chukwu akifunga la kwanza dakika ya 32 kabla ya Deus Kaseke kufunga la pili dakika ya 42.
  Na kipindi cha pili kilikuwa kigumu na wakati wengi wakiamini mchezo utamalizika kwa sare ya 2-2, kiungo Kenny Ally Mwambungu akawainua vitini mshabiki wa Lipuli kwa kufunga bao la ushindi dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90z a kawaida za mchezo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WANG’ARA NAMFUA, WAICHAPA 3-2 MWADUI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top