• HABARI MPYA

    Tuesday, January 10, 2017

    TIMU 48 SASA KUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA, ZIKIWEMO TISA ZA AFRIKA

    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeongeza idadi ya timu za kushiriki Kombe la Dunia hadi kufika 48 kuanzia Fainali za mwaka 2026 baada ya kura zilizopigwa mjini Zurich, Uswisi.
    Mpango huo uliobarikiwa na Rais Gianni Infantino, unamaanisha michuano hiyo sasa itaanza na makundi 16 ya timu tatu, huku mbili za juu zikienda hatua ya mtoani ya 32 Bora.
    Awali, Infantino alipendekeza kwamba FIFA ingetambulisha mikwaju ya penalti baada ya mechi ya makundi inayoisha kwa sare ili kuepuka mtindo wa timu kupata matokeo sawa. Kutakuwa na jumla ya mechi 80 katika mfumo mpya kutoka mechi 64 katika mfumo wa sasa wa timu 32.

    Ujerumani ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia baada ya kutwaa taji hilo mwaka 2014  

    Lakini iwapo timu itashika nafasi ya nne katika michuano ya 2026, itakuwa imecheza mechi saba sawa na mfumo wa timu 32 katika Kombe la Dunia.
    Kulikuwa pia kuna pendekezo kwa Wajumbe 37 wa Baraza la FIFA kupigia kura timu 40 kushiriki michuano hiyo, zigawanywe katika makundi 10 ya timu nne nne, au nane ya timu tano tano, lakini ni pendekezo la timu 48 lililokubalika.
    Nafasi za timu za Ulaya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitaongezeka kutoka 13 hadi 16, wakati Afrika na Asia zitaingiza timu tisa tisa kila Bara kutoka tano kwa Afrika na nne za Asia. 
    Maamuzi mengine kuhusu Fainali za 2026 - nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo yatafanyika mwaka 2020 huku kukiwa na ombi la kufanya pamoja baina ya Marekani no mojawapo au zote nchi za Canada na Mexico.
    Ongezeko la timu linamaanisha pia kutakuwa ongezeko la mapato kwa FIFA kutoka Pauni Milioni 521 hadi Bilioni 5.29 katika mfumo wa timu 48. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU 48 SASA KUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA, ZIKIWEMO TISA ZA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top